http://swahili.cri.cn/1/2007/12/03/1@68232.htm

Pyongyang-Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Christopher Hill aanza ziara nchini Korea ya Kaskazini

cri

Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambaye pia ni kiongozi wa ujumbe wa Marekani katika Mazungumzo ya Pande Sita kuhusu suala la Nyuklia la Peninsula ya Korea Bw. Christopher Hill amefika huko Pyongyang, mji mkuu wa Korea ya Kasazini na kuanza ziara yake ya siku tatu nchini Korea ya Kaskazini.

Bw. Hill amesema kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kumeingia mwishoni mwa kipindi cha pili, lazima kuhakikisha kuwa suala hilo linapata matokeo mazuri. Siku hiyo, Bw. Hill atakwenda sehemu ya Yongbyong na kufahamishwa hali ya mchakato wa kuondoa uwezo wa zana za nykulia. Baadaye atafanya mazungumzo na Bw. Kim Kye-gwan ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Korea ya Kaskazini katika mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la Pensinsula ya Korea, na naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea ya Kaskazini.

Bw. Hill amesema atafanya mazungumzo na Bw. Kim Kye-gwan kuhusu suala la kutekeleza jukumu linalopaswa kubebwa na kila upande, lakini hawatazungumzia suala kuhusu Marekani kujenga kituo cha mawasiliano nchini Korea ya Kaskazini. Alisisitiza kuwa sharti la kwanza ni Korea ya Kaskazini kuondoa uwezo wa zana za nyuklia ili kuufanya uhusiano kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini uwe wa kawaida.